Loading...

Kauli ya TFDA kuhusiana na habari zinazodai kuwa soda ya Novida ina virusi vya Ebola

Mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA) imewataka wananchi kupuuza taarifa ambazo zimekuwa zikisambazwa kwa nyakati tofauti kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna soda aina ya ‘Novida’ kutoka nchini Nigeria zimeingizwa nchini kinyemela na zina sumu ya virusi vya Ebola na tayari zimesababisha vifo vya watu 180 nchini humo.

Taarifa ya Mamlaka hiyo iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni mwendelezo wa taarifa yake ya awali iliyotolewa mwezi Aprili 2017 inabainisha kuwa taarifa zinazosambazwa za kuingizwa soda zenye sumu ya Ebola haina ukweli na inapaswa kupuuzwa.

Kwenye taarifa hiyo, TFDA imeeleza kuwa inatambua uwepo wa soda ziitwazo Schweppes Novida zinazozalishwa na viwanda vya Coca-Cola Kwanza,Bonite na Nyanza Bottlers na soda hizo zinazalishwa kwa kuzingatia mifumo bora ya uzalishaji na zinakidhi vigezo vya usalama na ubora.

"Kama ilivyo kwa bidhaa nyingize za chakula,vipodozi,vifaa vya tiba na vitendashi,soda za Schweppes Novida ambazo zimesajiliwa na TFDA zimekuwa zikifuatiliwa katika soko kupitia mifumo liyopo ya udhibiti ili kujiridhisha kuwa zinaendelea kukidhi vigezo vya usalama na ubora kwa lengo la kulinda afya ya mlaji," inabainisha sehemu ya taarifa ya TFDA . 

Soda aina ya Schweppes Novida kwa hapa nchini ilizinduliwa mwaka 2013, inatengenezwa na kusambazwa na viwanda vya Coca-Cola vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya na Kilimanjaro.Soda hizi zinazopendwa na wateja zinatengenezwa kwa ujazo wa ml 300 na ml 500 zipo za aina ya Mandarin Cooler zenye ladha murua ya machenza na Pineapple Breeze zenye ladha ya Nanasi.
Kauli ya TFDA kuhusiana na habari zinazodai kuwa soda ya Novida ina virusi vya Ebola Kauli ya TFDA kuhusiana na habari zinazodai kuwa soda ya Novida ina virusi vya Ebola Reviewed by Zero Degree on 5/21/2017 06:43:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.