Magogo yaliyokamatwa na Wakala wa Misitu Tanzania [TFS] kupigwa mnada
Magogo ya miti mbalimbali ambayo yalivunwa kinyume cha sheria ya misitu, kisha kukamatwa na Serikali kuhifadhiwa katika maeneo mbalimbali ya Kanda ya Magharibi sasa yanapigwa mnada na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Meneja wa Kanda ya Magharibi wa TFS, Juma Mwangi alisema magogo hayo baada ya kutaifishwa na Serikali yanayotarajiwa kuuzwa yana jumla ya mita za ujazo 4,511 ambayo ni sawa na tani milioni 4.51.
Alisema wafanyabishara kadhaa walitelekeza magogo hayo baada ya Serikali kipiga marufuku usafirishaji wa mazao ya misitu ikiwemo mkaa ambapo mfanyabiashara anayefanya biashara hiyo, atapaswa kuwa na vigezo ambavyo Serikali inavihitaji, tofauti na hapo sheria itachukua mkondo wake.
“Magogo ni pamoja na yale ya miti Mkulungu (Pterocarpus tinctorius) na magogo ya Mseni yatauzwa Mei 24 mwaka huu kwenye maeneo yalipohifadhiwa, yapo kwenye wilaya ya Sikonge, mengine Kaliua, Mlele, Mpanda na Tanganyika,” alisema Mwangi.
Magogo yaliyokamatwa na Wakala wa Misitu Tanzania [TFS] kupigwa mnada
Reviewed by Zero Degree
on
5/22/2017 11:58:00 PM
Rating: