Loading...

Sakata la vitabu feki lawaponza vigogo wawili wa Taasisi ya Elimu Tanzania [TIE]

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako leo Jumatatu jioni amewasimamisha kazi Kaimu Kamishna wa Elimu, Nicholas Bureta na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Tanzania (TIE), Dr. Elia Kidga kufuatia sakata la kasoro zilizopo katika vitabu vya kujifunzia wanafunzi.

Waziri Ndalichako ametangaza hatua hiyo kufuatia kuibuka kwa mjadala bungeni leo jioni kuhusu kasoro kwenye vitabu hivyo ambavyo vimechapishwa na taasisi hiyo kwa ajili ya kufundishia. Miongoni mwa makosa yaliyobainika kwenye vitabu hivyo, ni kurasa ulioandikwa kuwa Dodoma ndio mji mkubwa Tanzania.

Waziri Ndalichako amewasimamisha viongozi hao na ameliambia bunge kuwa uchunguzi wa kina unafanyika na baada ya kukamilika hatua za kinidhamu na kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika.

Wabunge walitishia kuzuia kupitisha bajeti ya Wizara ya Elimu hadi hapo wizara itakapotoa uamuzi wenye mantiki katika kutatua tatizo hilo lililozua mvutano mkubwa.

“Kwa mamlaka niliyonayo, namuagiza Kaimu Kamishna wa Elimu na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE), kuondoka ofisini mara moja ili kupisha uchunguzi,” alisema Ndalichako.

Baada ya waziri kutoa agizo hilo, wabunge waliridhia kupitisha bajeti ya wizara hiyo.
Sakata la vitabu feki lawaponza vigogo wawili wa Taasisi ya Elimu Tanzania [TIE] Sakata la vitabu feki lawaponza vigogo wawili wa Taasisi ya Elimu Tanzania [TIE] Reviewed by Zero Degree on 5/16/2017 09:56:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.