Loading...

Ujumbe wa Edward Lowassa kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa amewatakia mfungo mwema wa Ramadhani Waislamu wote akiwaomba kutumia ibada zao kuwaombea viongozi wa nchi hekima na busara na kuombea nchi amani na utulivu.

Waumini hao wanatarajiwa kuanza mfungo mtukufu wa Ramadhani Jumamosi baada ya mwezi kuandama.

Lowassa amesema kuanza kwa mfungo huo ni kutekeleza moja ya ibada zao muhimu kwa waumini hao.

“Ni kipindi ambacho Waislamu wanatakiwa kutenda mema zaidi na kuwa karibu zaidi na mwenyezi Mungu kwani malipo katika mwezi huu ni mara dufu zaidi ya miezi mingine.” 

“Nachukua nafasi hii kuwatakia ndugu zangu Waislamu mfungo mwema katika mwezi huo mtukufu wa Ramadhani, na kuwaomba wafanyabiashara kutopandisha bei za vyakula katika mwezi. Pia nawaomba ndugu zetu wakristo na wa dini nyingine kuwa na ushirikiano na wenzao kama ilivyo desturi yetu, ili watimize ibada hii muhimu kwao.” 

“Kwa wale wenye uwezo tuwasaidie wenzetu wasiyokuwa nao na pia katika ibada zetu tuiombee nchi yetu amani na utulivu na pia kuomba hekima na busara zitawale ndani ya vichwa vya viongozi wetu,” amesema Lowassa.
Ujumbe wa Edward Lowassa kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani Ujumbe wa Edward Lowassa kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani Reviewed by Zero Degree on 5/25/2017 02:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.