Loading...

Wafungaji bora waliokosa ubingwa barani Ulaya msimu huu

Wanasema mabao ni damu katika maisha ya soka na timu iliyofunga mabao mengi basi inanafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.


Hatahivyo, hakuna klabu yoyote iliyotwaa ubingwa katika ligi sita bora Ulaya, Hispania, Uingreza, Ujerumani, Italia, Ufaransa, na Ureno ambako bingwa wake wametoa mfungaji bora msimu huu 2016/17.

Hispania

Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi amefunga mabao 37, ndiye mchezaji aliyefunga

mabao mengi zaidi LaLiga, lakini Real Madrid wametwaa ubingwa.

Nafasi ya pili kwa ufungaji alikuwa Luis Suarez wa Barca aliyefunga mabao 29.

England 

Ulikuwa ni msimu mzuri wa Ligi Kuu England kwa mshambuliaji Harry Kane aliyemaliza akiwa

mfungaji bora na Spurs ikimaliza nafasi ya pili huku Chelsea ikitwaa ubingwa.

Mshambuliaji huyo wa Tottenham alifunga mabao nane mwezi Mei, mara ya mwisho kwa

mchezaji kufunga idadi hiyo ya mabao kwa mwezi alikuwa Luis Suarez akiwa na Liverpool miaka minne iliyopita akifunga mabao 10 kati 29.

Kane alimpita Romelu Lukaku aliyemaliza na mabao 25 na nyota wa Chelsea, Diego Costa aliyefunga bao 20.

Ujerumani

Mchezaji mwingine aliyevunja rekodi ya kihistoria ni Pierre-Emerick Aubameyang.

Mshambuliaji huyo alifunga mabao 31 akiwa na Borussia Dortmund, na kumpita Robert  Lewandowski aliyefanikiwa kuchukua ubingwa na Bayern Munich.

Italia

Baada ya miaka miwili kupita bila ya kufunga, Dzeko (31), amefanikiwa kuwa mfungaji bora wa  Serie A kwa mabao 29.

Mshambuliaji huyo wa Roma alikuwa na msimu mzuri, lakini Juventus ndio imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Italia.

Ufaransa

Baada tu ya Ibrahimovic kuondoka Paris Saint-Germain, majukumu yake yakabaki wa Edinson Cavani.

Mshambuliaji huyo wa Uruguay ameliziba pengo vizuri kwa kufunga mabao 35 katika Ligue 1, lakini hayakutosha kuizuia Monaco kutwaa ubingwa.

Ureno

Bas Dost amefanya vizuri katika misimu wake wa kwanza Ureno, akiwa amefunga mabao 34 katika mechi 31, alizocheza na Sporting Lisbon.

Pamoja na mabao hayo bado timu yake haikutwaa ubingwa na kuishia nafasi ya pili.
Wafungaji bora waliokosa ubingwa barani Ulaya msimu huu Wafungaji bora waliokosa ubingwa barani Ulaya msimu huu Reviewed by Zero Degree on 5/30/2017 11:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.