Loading...

Walimu wasusia Mei Mosi kisa ikiwa ni kukosa sare

WALIMU wa shule mbalimbali za msingi na sekondari wilayani Muheza mkoani Tanga, jana walisusia sherehe ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, kutokana na kukasilishwa na kukosa fulana ambazo hutolewa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kila mwaka.

Watumishi bora wa idara mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Muheza wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya hiyo jana katika sherehe za Meimosi katika uwanja wa jitegemee wilayani hapo.

Hali hiyo ilijitokeza jana katika sherehe hizo zilizofanyika uwanja wa Jitegemee wilayani hapa, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya,
Mwanasha Tumbo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Luiza Mlelwa, alisimama na kueleza kwamba amebaini kuwa walimu wengi hawakuwapo uwanjani na kuwa amepata taarifa wamesusa baada ya kukosa sare za Mei Mosi za mwaka huu.

Alisema kuwa anawaomba chama cha walimu wilaya ya Muheza kuhakikisha wanatengeneza sare hizo ili walimu waweze kupata kwa kuwa mwaka huu
inaelekea walimu hao wamenuna kwa kukosa sare, kitu ambacho si kizuri.

Mwenyekiti wa CWT wilaya ya Muheza, Mohamed Seif, alisema kuwa chama chao kimweka utaratibu wa kutoa fulana kwa walimu hao baada ya miaka miwili miwili kutokana na garama za uchapishaji.

Alisema mwaka jana 2016 walitoa fuana kwa walimu hao, lakini kutokana na utaratibu waliouweka kwamba mwaka huu hawatoi sare hizo kwa walimu mpaka mwaka 2018.

Source: Nipashe
Walimu wasusia Mei Mosi kisa ikiwa ni kukosa sare Walimu wasusia Mei Mosi kisa ikiwa ni kukosa sare Reviewed by Zero Degree on 5/02/2017 05:16:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.