Loading...

Beyonce Knowles ajifungua mapacha


Nyota wa muziki wa Pop nchini Marekani Beyonce amejifungua mapacha kulingana na vyombo vya habari vya nchini Marekani.

Vyombo vya habari vya Entertainment Weekely, Us Weekly na People Magazine vimethibitisha habari hizo lakini tarehe ya kuzaliwa na jinsia ya watoto haijajulikana.


Beyonce ambaye ni mke wa mwanamuziki wa Rap, Jay Z alitangaza kwamba ni mjamzito katika picha ya Istangram mnamo mwezi Februari ambapo ni picha iliopendwa mno katika historia ya mtandao huo.

Wawili hao tayari wana mtoto wa kike, kwa jina anaitwa Blue Ivy aliye na umri wa miaka mitano.

Hakujawa na taarifa rasmi kuhusu kujifungua huko kutoka kwa Beyonce na Jay Z mwenyewe.

Picha ya Beyonce akiogelea chini ya maji wakati akiwa mjamzito
Picha nyengine zilizochapishwa na Beyonce baada ya kutangaza kuwa ni mjamzito ziliomuonyesha akiogelea chini ya maji, akiwa katika maua huku akiwa amekaa uchi ndani shada la maua.

Katika picha moja mwimbaji huyo wa wimbo 'Lemonade' alisimama akiwa uchi na kushikilia tumbo lake na mkono mmoja na mwengine akishikilia titi lake , mbele ya kichwa cha kiongozi wa zamani wa Msiri.
Beyonce Knowles ajifungua mapacha Beyonce Knowles ajifungua mapacha Reviewed by Zero Degree on 6/18/2017 08:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.