Loading...

Conte amtimua Diego Costa Chelsea kwa ujumbe wa simu


Diego Costa amesema kwamba Antonio Conte amemtumia ujumbe kupitia simu yake unaomweleza kwamba hayupo katika mipingo yake kwa msimu ujao Chelsea.

Kocha huyo wa mabingwa wa Ligi Kuu England, Antonio Conte amemuandikia ujumbe mshambuliaji wake, Diego Costa kuwa hamhitaji.

Awali ilionekana Costa angeweza kurejea Atletico Madrid lakini sasa wamezuiwa kusajili.

Costa raia wa Hispania ndiye aliyetoa siri hiyo wakati akihojiwa na kusema Conte kamuambia hamhitaji.

“Kaniandikia ujumbe, kasema hanihitaji, hajanijumuisha katika mipango ya msimu ujao,” alisema Costa raia wa Hispania.


Nyota huyo mwenye miaka 26 amefunga mabao 26 katika michezo 46 aliyoichezea Chelsea msimu huu na amekuwa akihusishwa na kuondoka Stamford Bridge miezi kadhaa iliyopita, kwa mara ya kwanza ilikuwa Atletico Madrid, kisha akahusishwa na kuhamia Ligi kuu ya China, kisha yeye mwenyewe akadai atakuwepo klabuni, sasa ni ajabu kulingana na jinsi mambo yalivyogeuka, Costa ataondoka Chelsea kama ilivyothibitika.

Kocha huyo Muitaliano anaonekana kuelekeza nguvu zake kwa mshambulizi Romelu Lukaku kutoka Everton.
Conte amtimua Diego Costa Chelsea kwa ujumbe wa simu Conte amtimua Diego Costa Chelsea kwa ujumbe wa simu Reviewed by Zero Degree on 6/08/2017 01:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.