Loading...

Emmanuel Okwi, Simba mambo yako vizuri, Manara asema dili limetiki

Mshambuliaji Ibrahim Ajib yupo njiani kukamilisha mchakato mzima wa kuelekea Yanga akitokea Simba, hiyo siyo habari nzuri kwa Wanasimba lakini kuna taarifa njema kwao.

Mwenyeki wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe (kulia) akiwa na Emmannuel Okwi.
Habari kutoka ndani ya Klabu ya Simba inaeleza kuwa klabu hiyo ipo kwenye hatua za mwisho za kumvalisha Emmannuel Okwi jezi namba 25 ambayo alikuwa kiitumia kikosini hapo kama usajili wake utakamilika.

Okwi ambaye ameshaitumikia Simba kwa vipindi viwili tofauti, inadaiwa kuwa alitua jijini Dar es Salaam, inasemekana alikutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe na kumalizana mjini Kampala.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Haji Manara ambaye alikuwa Ofisa Habari wa Simba, ameweka picha ya Okwi akiwa na Mwenyeki wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe kisha kuandika ‘DEAL DONE’, ikionekana anamaanisha kila kitu kimekamilika.
Emmanuel Okwi, Simba mambo yako vizuri, Manara asema dili limetiki Emmanuel Okwi, Simba mambo yako vizuri, Manara asema dili limetiki Reviewed by Zero Degree on 6/16/2017 08:59:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.