Loading...

Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 08


MTUNZI: MC Short Charles Gwimo

Ilipoishia..........Mgeni rasmi alituasa mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya, utoro wa darasani na tusiyavamia mapenzi katika umri mdogo kwani kufanya hivyo ni sawa na kuyafumania mapenzi na kuwa FUMANIZI LA MAPENZI. Alihitimisha hotuba yake kwa kuwaonya vijana wenye mtindo wa kushiriki mapenzi ya jinsia moja kwa kuwaambia athari zake ambazo ni kulegea kwa misuli ya mwaranda au kupata kansa ya mlango wa haja kubwa. Na hapa alikuwa anawazungumzia mabasha walioibuka shuleni kwetu ingawa hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja.

Endelea nayo: Awamu ya kwanza ya sherehe ilihitimika salama kwa wanafunzi wote na wageni kushiriki chakula cha pamoja huku tukisubiri kwa hamu awamu ya pili ambayo wanafunzi wengi huiona ya muhimu kwani huambatana na disko. Baada ya chakula niliamua kujitenga mbali na wenzangu ili nifanye tathimini ya zawadi nilizotuzwa. Moyoni niliwaza kupokea zawadi kama vile pesa ambazo nilianza kuzifanyia bajeti za matumizi ya shule vikiwemo vitafunwa. Mawazo yangu yaligeuka ghafla na kuwa huzuni mara nilipofungua bahasha ya kwanza na kukutana na zawadi ya mipira miwili ya kiume almaarufu kama kondomu. Naam! Limbukeni wa mapenzi nimekutana na kituko cha mwaka. Nilijipiga moyo konde kuendelea kuchakura vizawaadi vyangu lakini sikuambulia chochote zaidi ya vimemo vyenye maneno mvuto wa mapenzi kama vile, “Maneno yako yaendane na vitendo mimi ni wako”, “Natamani uwe wa kwanza kunitoboa kizinda hata kwa ncha ya ulimi” na kengine ; “Tumekuja wengi ila bikra ni bikira ni mimi wengine dampo la manispaa” ……hayo ni baadhi ya maneno niliyokutana nayo kwenye zawadi nilizotuzwa nikiwa uwanjani. Vingine nilivyofaidi ni pipi za kijiti au alamba kama wasemavyo watoto wa kileo. 


**********


Mnamo saa mbili kamili usiku, eneo lolote la mazingira ya shule lilizagaa kwa mitindo tofauti ya mavazi. Ungebahatika kuyatembelea mazingira hayo kwa usiku huo, nahisi ungedhani kuna hafla ya maonesho ya mavazi kwani walikuwepo waliokuwa wamepigilia vipedo, vimini, charanga, vibana misulu ambavyo siku hizi wanaviita kwa jina la “kamatia chini” na kuna mavazi mengine ambayo mpaka sasa siyafahamu kwa majina. Kina dada walikuwa wametokelezea kinoma huku wengine wamejipodoa kwa kujipaka wanja kwa mtindo ule maarufu wa “mtoto sina mume”. Rangi za midomo zilisanifiwa kulingana na wajihi wa mtu na muonekano wa mavazi yake. Kwa kuwa ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kuvishuhudia vimbwanga kama hivyo, nilijiweka karibu sana na Mood aliyeonekana kuwa ni mzoefu wa mambo hayo kunizidi ili nisionekane wa kimbiji au sigimbi kijijini.


**********


Tulijimwaga ukumbini huku mimi nikiwa mtazamaji wa wacheza muziki niliyejikalisha kwenye viti vya nyuma kabisa ili nione jinsi wenzangu wanavyosakata muziki. Dj Shuku kijana mmiliki wa saloon maarufu kwa jina la “God bless Hair Cutting” ndiye aliyekuwa akitupia michomo mbali mbali ndani ya ukumbi. Dj aliweza kuipangilia miziki yake kwa umaridadi mkubwa kwa kucheza nyimbo zile za kikongo hadi zile za “MAMTONI” bila kuzisahau Bongo fleva za hapa hapa nyumbani Tanzania. Wachezaji walikuwa wakicheza kwa mitindo mbali mbali ya kuchekesha na isiyochekesha. Kuna waliokuwa wakicheza mithili ya ngono za kisukuma za kipindi cha mavuno maarufu kama “Chagulaga” na wengine wakirukaruka kama walevi wa msopagi au komoni pembe ya Wahehe. Pia walikuwepo wale ambao walivitumia viuno vyao kuvizungusha bila mpangilio kama feni mbovu na wako waliokuwa wamebarikiwa kuvizungusha viuno vyao kama pia ilimradi tu disko linachezwa kiroho safi. Nikiwa nimejibanza nyuma kabisa ya ukumbi kwenye viti vilivyopangwa kwa minajili ya watazamaji na wapumzikaji, pembeni yangu alikuja kukaa binti mmoja ambaye baadaye nilikuja kumtambua kwa jina la SHAMIA. Nikiwa nimevalia boshori langu kichwani ili nisionekane vizuri mule ukumbini, niliweza kuwaona wakina dada wengi wakizunguka zunguka kwa malengo ya kuwatafuta ‘partners’ wa kucheza nao. Nilishangazwa na mitindo ya kuombana kucheza muziki kwa kuiweka mikono kifuani kisha kumuinamia kidogo Yule umtakaye naye akiridhia husimama na kuanza kucheza pamoja. Ama kweli, ushamba siku zote ni mzigo ingiwa hauna uzani. Niliendelea kushangaa kwa muda mrefu hadi pale rafiki yangu Mood alipokuja kunishtua, “Vipi Devi, mbona hauchezi muziki kulikoni?” Alivyoniita tu kwa jina, nilishangaa binti aliyekuwa amekaa pembeni yangu akihamaki kwa kushusha pumzi mithili ya kuli aliyekuwa ameelemewa na gunia la mchele bandarini. Nilimjibu mudi kuwa, “Muda ukitimu nitajimwaga tu uwanjani”. Mood aliendelea kujirusha na mabinti tofauti tofauti mle ukumbini huku akiwa amejaa nyemi kupindukia.


**********


Nikiwa katika hali tafakuri kwanini dada Yule alihamaki ghafla Mood alipolitaja jina langu, mara akaibuka mwanadada aliyejipigilia kimini cheusi kilichoyaacha mapaja yake meupe pe! Na malaini yakiwa katika hali ya utupu. Mvao wake ulinifanya nipandwe na ashiki bila kutegemea. Alipofika maeneo yetu, alinikazia sana macho lakini hakuambulia chochote kutoka kwangu zaidi ya kumtambua kimwana aliyekuwa amekaa pembeni yangu. Pasina hata salamu alianza kumchamba na kumchambua Yule dada aliyekuwa pembeni yangu kwa kumtaja kwa jina na mimi nikapata wasaa wa kulijua. “Ama kweli disko limeingiliwa, hata walokole kama SHAMIA mmeingia? Ndiyo maana hata Devid handsome boy wangu ameligomea kwa kuwa nyumba ya shetani mwendawazimu kajikaribisha sebuleni”. Aliendelea kumzodoa, “Umejifanya kutulia viti vya nyuma kama mtoto mwema kumbe paparazzi uliojaa ushambenga kwa kuandika yasiyokuhusu, sasa ole wako ukatutoe magazetini tutakaporudi Kibondo ndiyo utanijua jina la ‘Tipha’ nililirithi kutoka kwa nani. Acha sisis tunaojua thamani ya bustani inayomwagiliwa na mabomba ya Kijerumani. Utabakia hivyo hivyo na shamba linaloogopa kumwagiliwa kwa mabomba laini yenye kutia mashamsham”. “Halo halo disko limeingiliwa”. Tipha alimalizia mipasho yake kwa mbwembwe kisha akapotelea ukumbuni. Nilianza kujisogeza taratibu kuelekea uelekeo wa Shamia ambaye nilihisi kuwa yeye ni mmoja wa wale walionipa zawadi ya vimemo ili niweze kumtupia ndoano yangu yenye chambo mfu. Kikubwa kilichomfanya nijisogezee kwa Shamia ni moja ya kimemo nilichokisoma miongoni mwa zile zawadi nilizotunzwa ukumbini kikizungumzia suala la ubikira. Nilitamani niwe wa kwanza kukitoboa kizinda chake ambapo atakuwa ni muhusika. Nilipokuwa nikiendelea kujisogeza kwa Shamia, aliniachia jicho la mkonyezo likimaanisha kuwa “Sogea tu hata mimi nilikuwa naisubiri nafasi kama hiyo”. Moyoni nilitamani sana nipate bahati ya kukizindua kibustani chake kwa kuwa wa kwanza kutia jembe langu na kuweka historia ya mahusiano mabichi ya tendo la ndoa kwani waswahili husema, “Utamu wa pasheni jichumie, ukatiwe kisha tia kidole cha kati ndipo ule”. Mate yalianza kunijaa mdomoni huku athumani kichwa wazi wangu akiendelea kuutafuta upenyo wa kujitoa kwenye joto lisilo na manufaa aingie kwenye pango lenye manufaa.

====>>Itaendelea ijumaa ijayo...



Usiikose SEHEMU YA 09>>> ya Riwaya hii ifikapo Ijumaa ya wiki hii, na utaipata hapa Zero Degree pekee.
Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 08 Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 08 Reviewed by Zero Degree on 6/26/2017 01:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.