Loading...

Mtazamo wa Kichuya juu ya suala la Simba kuwasajili Bocco, Kapombe na Aishi Manula


Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya amesema anaamini timu yake itafanya vizuri kutokana na usajili inaofanya.

Simba imesajili wachezaji saba hadi sasa akiwemo Ally Shomari kutoka Mtibwa Sugar, John Bocco, Shomari Kapombe na Aishi Manula waliosajiliwa kutoka Azam FC. 

Kichuya ambaye alikuwa mfungaji bora wa Simba msimu uliopita alisema wachezaji wapya wataleta changamoto kikosini.

“Ni usajili mzuri ambao utaongeza changamoto kwenye timu, naamini tutakuwa na timu nzuri msimu ujao kwa kuwa wachezaji waliosajiliwa ni wazoefu na Ligi,” alisema Kichuya aliyefunga mabao 12 katika Ligi Kuu na kuiwezesha Simba kushika nafasi ya pili na kuchukua ubingwa wa Kombe la FA.
Mtazamo wa Kichuya juu ya suala la Simba kuwasajili Bocco, Kapombe na Aishi Manula Mtazamo wa Kichuya juu ya suala la Simba kuwasajili Bocco, Kapombe na Aishi Manula Reviewed by Zero Degree on 6/20/2017 10:37:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.