Loading...

Mwalimu ajiua katika nyumba ya kulala wageni


MWALIMU Betson Sanga aliyekuwa akifundisha Shule ya Sekondari Milundikwa wilayani Nkasi mkoani Rukwa, amefariki dunia baada ya kunywa sumu akiwa katika nyumba moja ya kulala wageni.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando, alisema jana mwalimu huyo alifariki dunia juzi usiku akiwa ndani ya chumba alichokuwa amepanga katika nyumba ya kulala wageni iliyopo eneo la stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani. 

Kyando alisema mwalimu huyo aliacha ujumbe usemao "kama nadaiwa deni lolote na mtu amweleze mkurugenzi ambaye ni mwajiri wangu, lakini asilaumiwe chochote juu ya kifo changu."

Inasemekana siku ya tukio mwalimu huyo alifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni na kupanga chumba kwa ajili ya kulala kisha alikabidhi funguo na kuondoka kuelekea kusikojulikana.

Taarifa zinadai ilipofika usiku wa manane, marehemu alirejea katika nyumba hiyo akiwa amelewa na kuchukua funguo kwa mhudumu kisha kuingia ndani ya chumba chake kulala.

Baadaye mhudumu wa nyumba hiyo alisikia sauti ya kukoroma kwa sauti ya juu, hali iliyomtia wasiwasi na alipokwenda kumgongea, hakufungua mlango kwa muda mrefu huo na ndipo alipoomba msaada kwa wapangaji wengine ili kumsaidia kuvunja mlango.

Walipoingia ndani ya chumba hicho walimkuta akiwa anatokwa na povu mdomoni na kumkimbiza hospitali, lakini alifariki dunia wakiwa njiani.

Kwa mujibu wa Kamanda Kyando, uchunguzi wa kitabibu ulibainisha mwalimu huyo alijiua kwa kunywa sumu.
Mwalimu ajiua katika nyumba ya kulala wageni Mwalimu ajiua katika nyumba ya kulala wageni Reviewed by Zero Degree on 6/28/2017 10:17:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.