Loading...

Sasa ni rasmi, Ibrahim Ajibu ni mchezaji wa Yanga SC


Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu imefahamika kuwa sasa ni rasmi anajiunga na Yanga baada ya klabu yake ya sasa kushindwa kufikia nae makubaliano ya kumbakiza kwenye kikosi.

Mabosi wa Simba na mchezaji huyo wameshindwa kuafikiana juu ya makubaliano ya mkataba wake mpya na hiyo imewapa nafasi Yanga waweze kumchukua.

Taarifa kutoka ndani ya Simba imeeleza kuwa wameamua kumruhusu aondoke baada ya mchezaji huyo kuonyesha kutokuwa na nia ya kuendelea kubaki klabuni hapo.

“Tumemwacha aende anakotaka kwenda kwa sababu hana ‘spirit’ tunayoihitaji sisi, acha aende tu sisi mbele kwa mbele,” amesema mtoa taarifa.

Ajib ambaye alianza kutamba Simba akitokea kikosi cha vijana, atatua Yanga akiwa mchezaji huru kutokana na mkataba wake kuelekea mwishoni.

Ifahamike kwamba, Ibrahim Ajibu, hataipata jezi aliyokuwa anaitumia Simba na tayari ameshauriwa kutafuta namba nyingine na si 23 ambayo inatumiwa na Mkongwe wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Ajibu amesaini Yanga miaka miwili na usajili wake umezuia gumzo huku ukiamsha morali ya Wanayanga ambao walionekana kukata tamaa wakati Simba ikisajili mfululizo.

Jezi namba 23 upande wa Yanga tayari inaonekana ina mwenyewe. Cannavaro anajulikana kama “Baba Mwenye Nyumba”.

Hii inatokana na kuwa Yanga kwa muda mrefu pia ni kati ya manahodha wa muda mrefu.
Sasa ni rasmi, Ibrahim Ajibu ni mchezaji wa Yanga SC Sasa ni rasmi, Ibrahim Ajibu ni mchezaji wa Yanga SC Reviewed by Zero Degree on 6/16/2017 12:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.