Loading...

Simba SC, Jang'ombe Boys wametupwa nje ya michuano ya 'SportPesa Super Cup'

Simba SC vs Nakulu All Stars
Gor Mahia imekuwa timu ya pili ya Kenya kutinga nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup.

Jang'ombe Boys
AFC Leopards ndiyo timu ya kwanza ya Kenya kufuzu nusu fainali baada ya kuishinda Singida United na itacheza na Yanga hatua ya nusu fainali.

Gor Mahia imefuzu baada ya kuitwanga Jang’ombe Boys ya Zanzibar kwa mabao 2-0 katika mchezo wa robo fainali uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar.

Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere ndiye mfungaji wa mabao yote mawili katika dakika ya 66 na 78.

Gormahia
Sasa Gor Mahia wanasubiri mshindi kati ya Simba dhidi ya Nakuru All Stars ya Kenya pia ambao umeanza tayari.

Katika mchezo mwingine uliopigwa leo, Nakuru All Stars imefanikiwa kuwa timu ya tatu ya Kenya kutinga nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup.

Nakuru imeitwanga Simba kwa mikwaju ya penalti 5-4 na kutinga nusu fainali na sasa itacheza na Gor Mahia ya Kenya pia.

Dakika 90 kati ya Nakuru na Simba ziliisha kwa sare ya bila bao huku Nakuru wakionekana kupoteza nafasi nyingi zaidi.

Simba ilipewa nafasi ya kusonga kwa kuwa ni wazoefu na Nakuru si timu kubwa.

Simba iliwajaribu wachezaji kadhaa wakiwemo kutoka Rwanda lakini haikuonyesha makali sana.

Wakati wa upigaji penalti, wachezaji wawili wa kimataifa wa Simba, kipa Daniel Agyei ndiye aliyekosa penalti hiyo moja huku yeye akiruhusu zote tano kutinga wavuni.
Simba SC, Jang'ombe Boys wametupwa nje ya michuano ya 'SportPesa Super Cup' Simba SC, Jang'ombe Boys wametupwa nje ya michuano ya 'SportPesa Super Cup' Reviewed by Zero Degree on 6/06/2017 07:02:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.