Loading...

Ujerumani yatinga fainali ya Kombe la Mabara baada ya kutoa dozi nzito kwa Mexico


Ujerumani imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la mabara baada ya kuichapa bila huruma Mexico 4-1.

Leon Goretzka alifunga mara mbili katika mtanange huo katika dakika ya 6 na 8.

Magoli mengine ya Ujerumani yaliwekwa kimiani na Timo Werner dakika ya 59 na Amin Younes dakika ya 90.

Goli la kufutia machozi kwa upande wa Mexico lilipachikwa na Marco Fabian dakika ya 89.

Mexico walipata nafasi nyingi lakini hawakuweza kuzitumia vyema huku Ujerumani ikionekana kukomaa vilivyo katika safu ya ulinzi.

Fainali ya kombe la mabara itapigwa jumapili ya Julai 2 kati ya Ujerumani na Chile mjini St Petersburg, huku mchezo wa awali ukizikutanisha Ureno na Mexico kutafuta mshindi wa tatu.
Ujerumani yatinga fainali ya Kombe la Mabara baada ya kutoa dozi nzito kwa Mexico Ujerumani yatinga fainali ya Kombe la Mabara baada ya kutoa dozi nzito kwa Mexico Reviewed by Zero Degree on 6/30/2017 10:51:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.