Loading...

Umeisikia hii ya Kanisa lililofanya Ibada maalum kumshukuru Mungu kwa Chelsea kubeba Ubingwa?


Kanisa la Living Streams International lililopo Accra Ghana limeandaa na kufanya Ibada maalum kumshukuru Mungu kwa kuisaidia Chelsea F.C kumaliza vizuri msimu wa 2016/17 na kuibuka mabingwa wa Premier League.


Mchungaji wa Kanisa hilo ambaye ni shabiki mkubwa wa Chelsea aliwahamasisha waumuni wake kuvalia jezi za timu hiyo katika Ibada hiyo ambapo iliandaliwa keki maalum huku waumini wakiimba wimbo wa timu “Blue is the Colour”.

Mbali na hilo waumini wengine ambao sio mashabiki wa Chelsea waliruhusiwa kuvaa jezi za timu zao ambapo Mchungaji Mkuu ambaye ni shabiki wa Arsenal alialikwa kushiriki kwenye Ibada akiwaambia waumini lengo ni kutumia nguvu za soka kuzungumzia kuhusu Mungu.


Umeisikia hii ya Kanisa lililofanya Ibada maalum kumshukuru Mungu kwa Chelsea kubeba Ubingwa? Umeisikia hii ya Kanisa lililofanya Ibada maalum kumshukuru Mungu kwa Chelsea kubeba Ubingwa? Reviewed by Zero Degree on 6/06/2017 08:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.