Loading...

Umeisikia hii ya wavulana kuvaa sketi shuleni kupinga kuzuiliwa kuvaa kaptula Uingereza??

Wavulana wavaa sketi shuleni nchini Uingereza kupinga kunyimwa ruhusa ya kuvaa kaptula
Takriban wavulana 30 wamevaa minisketi kuenda shuleni wakiandamana kupinga, baada ya kuambiwa kuwa hakuruhusiwa kuvaa kaptula.


Wanafunzi hao walikuwa wameomba ruhusa ya kubadilisha sare zao kutokana na kupanda kwa viwango vya joto.

Mwalimu mkuu wa shule, Aimee Mitchel alisema kuwa kaptula hazikuwa kati ya sare za shule.

Wanafunzi walisema kuwa hatua ya kufanya maandanao ilitokea kwa mwalimu mkuu ambaye alikuwa ametoa pendekezo hilo awali, licha ya wanafunzi kusema walihisi hakumaanisha hivyo kasisa.

Wanasema wana matumaini kuwa shule itaangalia upya sera za kuvaa katptula kutokana maandamano hayo.

"Kaptula kwa sasa si sehemu ya sare zetu kwa wavulana na siwezii kufanya mabadiliko yoyote bila ya kuaomba ushauri wa wazazi na familia zao.

"Hata hivyo kutokana na kuwepo majira ya joto, ninatarajia kuwepo mabadiliko siku za usoni," Bi Mitchell alisema.
Umeisikia hii ya wavulana kuvaa sketi shuleni kupinga kuzuiliwa kuvaa kaptula Uingereza?? Umeisikia hii ya wavulana kuvaa sketi shuleni kupinga kuzuiliwa kuvaa kaptula Uingereza?? Reviewed by Zero Degree on 6/23/2017 02:46:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.