Loading...

Watu zaidi ya 120 wamepoteza maisha katika ajili ya moto Pakistan


Watu 123 wamefariki dunia baada ya lori la mafuta kupinduka na kulipuka katika mji wa Ahmedpur Sharqia, Punjap nchini Pakistan.

Vyombo vya habari vya nchini humo vimethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyogharimu maisha ya watu 123 huku wengine wakijeruhiwa vibaya.

Imeelezwa kuwa baadhi yao walipoteza maisha wakiwa wanajaribu kuteka mafuta kutoka kwenye lori hilo mara baada ya kupinduka. Majeruhi wamepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zinasema kuwa, lori hilo la mafuta lililokuwa likiendeshwa kwa kasi, lilipinduka, likaanguka na kisha kushika moto.

Hata hivyo mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa baadhi ya watu waliofika katika eneo la ajali mara baada ya gari hilo kupinduka walikuwa wakivuta sigara, jambo ambalo limeelezwa kuwa chanzo cha moto huo.

Source: BBC.
Watu zaidi ya 120 wamepoteza maisha katika ajili ya moto Pakistan Watu zaidi ya 120 wamepoteza maisha katika ajili ya moto Pakistan Reviewed by Zero Degree on 6/26/2017 01:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.