Loading...

Wenger amekuwa wa kwanza kutangaza ofa kwa Kylian Mbappe

Kylian Mbappe [Monaco]
Arsenal wanaweza wasifanikiwe kumnasa nyota wa Monaco, Kylian Mbappe, lakini mvutano utakuwa mkubwa katika mashindano ya kumsaka nyota huyo mwenye kipaji cha soka.

Mbappe
Mbappe ambaye kwa kiasi kikubwa amekuwa akifananishwa na shujaa wa zamani wa 'The Gunners', Thierry Henry, inaripotiwa kwamba anawindwa na Manchester City, Real Madrid na Arsenal ikijumuishwa, lakini Arsene Wenger amekuwa wakwanza kutangaza ofa.

Kwa mujibu wa taarifa ya L’Equipe, Arsenal wameweka ofa ya karibuni sawa na dola za kimarekani milioni 113 kumnasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 18, ambaye atatimiza miaka 19 mwezi desemba tarehe 20.

Kylian Mbappe akishangilia moja ya magoli aliyoifungia Monaco
Mbappe amefunga magoli 26 na kutoa 'assist' 14 msimu huu, sita kati ya hizo ni zile za mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya (sita zote zilipatikana wakati wa hatua ya mtoano).

Nyota huyo amesema haogopi kuondoka Monaco. Je, atajiunga pamoja na Henry na Wenger kuingia kwenye historia ya klabu ya Arsenal?
Wenger amekuwa wa kwanza kutangaza ofa kwa Kylian Mbappe Wenger amekuwa wa kwanza kutangaza ofa kwa Kylian Mbappe Reviewed by Zero Degree on 6/02/2017 04:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.