Loading...

AJALI: Watu 16 wafariki dunia kwenye ajali ya ndege ya jeshi nchini Marekani


Takriban watu 16 wamefariki kwenye ajali ya ndege ya jeshi kwenye jimbo la Mississipi nchini Marekani.

Ajali hiyo ilitokea katika kaunti ya LeFlore karibu kilomita 160 kusini mwa mji mkuu wa jimbo hilo, Jackson.

Watu wote 16 waliokuwa ndani ya ndege hiyo waliangamia.

Hakuna taarifa rasmi zilizotolewa kuhusu kilichosababisha kutokea ajali hiyo.

Kwa mujibu wa jarida la jimbo la Mississipi ni kuwa ndege hiyo ilianguka katika shamba moja na mabaki yake yakatabakaa mbali.
AJALI: Watu 16 wafariki dunia kwenye ajali ya ndege ya jeshi nchini Marekani AJALI: Watu 16 wafariki dunia kwenye ajali ya ndege ya jeshi nchini Marekani Reviewed by Zero Degree on 7/11/2017 09:04:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.