Loading...

Liverpool yaingia vitani dhidi ya Chelsea kusaka saini ya kinara wa mabao Dortmund


Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa leo, Chelsea na Liverpool wako katika vita ya kuwania saini ya nyota wa Borussia Dortmond, mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang.

Ripoti zinadai kwamba, Chelsea na Liverpool kwa nyakati tofauti tofauti wamefanya mazungumzo na Aubameyang kujaribu na kufunga makubaliono ya mkataba kabla ya kuweka mezani ofa ya paundi milioni 65.

Mtandao wa 'The Metro' umeripoti kwamba, Liverpool wanaweza kuwa na nafasi kubwa ya kumsajili Aubameyang kwa ajili ya uhusiano uliopo kati ya Dortmund na meneja Jurgen Klopp.

Raia huyo wa Gabon alifunga magoli 40 msimu uliopita kiasi cha kuzivutia klabu nyingi kubwa katika majira haya ya joto, na hivi karibuni amekuwa akihusishwa zaidi na kuhamia Stamford Bridge.

Ripoti nyingine mpya zinadai AC Milan na wanamatamanio makubwa ya kuipata saini ya nyota huyo na tayari wamekwishapeleka ombi lao Dortmund kuhusiana na dili la kumnasa Aubameyang.

Aubameyang amekuwa akihusishwa na kuondoka Ujerumani katika majira haya ya joto, na tayari klabu nyingi zimekwishaingia katika vita hiyo ya kuisaka saini yake kama ilivyotarajiwa.
Liverpool yaingia vitani dhidi ya Chelsea kusaka saini ya kinara wa mabao Dortmund Liverpool yaingia vitani dhidi ya Chelsea kusaka saini ya kinara wa mabao Dortmund Reviewed by Zero Degree on 7/14/2017 11:48:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.