Loading...

Mkulima auawa kwa kupigwa risasi 8 Kibiti


MKULIMA wa Kijiji cha Ruaruke wilayani Rufi ji mkoani Pwani, Ramadhani Mzuzuri (45) amefariki dunia kwa kupigwa risasi nane na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.

Mbali ya kumuua Mzuzuri, pia watu hao wamemjeruhi kwa kumpiga risasi tatu mke wa marehemu, Halima Mzuzuri. Akithibitisha mauaji hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Rufiji, Onesmo Lyanga alisema mbali ya kuua na kujeruhi, pia kuna taarifa kuwa watu watatu wametoweka. Kamanda Lyanga alisema polisi wanafanya uchunguzi ikiwemo kujua idadi ya watu wanaodhaniwa kutekwa.

Akizungumzia uchunguzi wa mwili wa marehemu Mzuzuri, Dk David Paul wa Kituo cha Afya Kibiti alisema katika uchunguzi walioufanya, walibaini kuwa marehemu alikuwa na majeraha manane mwilini mwake yaliyotokana na kupigwa risasi. Kwa upande wake, Daktari wa Hospitali ya Mchukwi, Dk Emmanuel Humbi alikiri kufikishwa hapo kwa mke wa marehemu kupatiwa matibabu ambapo alipokelewa akiwa hajitambui kutokana na kuwa na majeraha sehemu tatu tofauti.
Mkulima auawa kwa kupigwa risasi 8 Kibiti Mkulima auawa kwa kupigwa risasi 8 Kibiti Reviewed by Zero Degree on 7/11/2017 02:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.