Loading...

Msanii Bobi Wine kuapishwa kama mbunge nchini Uganda

Mwanamuziki wa nyimbo za reggae nchini Uganda Robert Kyagulanyi Ssentamu, maarufu kama Bobi Wine, anaapishwa leo kama mnunge wa eneo la Kyadondo East.

Wine aliwania kiti hicho kama mgombea huru na kuwashinda wagombea wanne ambapo alipata kura 25,659 kati ya kura 33,310 zilizopigwa
Wine aliwania kiti hicho kama mgombea huru na kuwashinda wagombea wanne ambapo alipata kura 25,659 kati ya kura 33,310 zilizopigwa kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika tarehe 29 mwezi Juni.

Alisema kuwa anaingia bungeni kama kiongozi na wala si mwanasiasa, kwa mujibu wa gazeti la New Vision.

Chama tawala NRM na upinzani wamekuwa wakimtaka Wine ajiunga na mmoja wao.

Picha ya Wine akimsalamia Rais Museveni wakati wa misa ya mfanyabiashara mmoja ilikosolewa na baadhi ya wafuasi wake katika mitandao.
Msanii Bobi Wine kuapishwa kama mbunge nchini Uganda Msanii Bobi Wine kuapishwa kama mbunge nchini Uganda Reviewed by Zero Degree on 7/11/2017 01:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.