Loading...

Ngeleja arudisha shilingi milioni 40.4 za Escrow


Mbunge wa Sengerema, Mheshimiwa WILLIAM NGLEJA ametangaza kurejesha Shilingi zaidi ya Milioni 40 Serikalini kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA- ambazo aliingiziwa kwenye akaunti yake na Bwana JAMES RUGEMALIRA kwa ajili ya kusaidia jimbo lake.

Mheshimiwa NGELEJA amesema ameamua kurejesha fedha hizo kutokana na hali iliyojitokeza kuwa fedha hizo kuwa siyo safi.

Amesema hayuko tayari kuwa sehemu ya viongozi wa jamii ambao watakuwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo rushwa na ubadhilifu wa fedha katika shughuli za Serikali.

Mbunge huyo wa Sengerema aliwaonesha stakabadhi Waandishi wa Habari aliokutana nao kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari - MAELEZO- za fedha hizo alizozirejesha Serikalini.

Bwana JAMES RUGEMALIRA anakabiliwa na kesi ya kuhujumu uchimi.
Ngeleja arudisha shilingi milioni 40.4 za Escrow Ngeleja arudisha shilingi milioni 40.4 za Escrow Reviewed by Zero Degree on 7/11/2017 07:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.