Loading...

Singida United yasajili nyota wawili toka Rwanda


Klabu ya Singida United jana iliwatambulisha wachezaji wengine wawili wa kimataifa kutoka nchini Rwanda ambao wameshasaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa miaka miwili.

Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga alisema wachezaji hao ambao ni Mishel Lishangoga ambaye ni beki aliyekuwa akiitumikia Klabu ya APR ya nchini Rwanda pamoja na Dany Usengimana akitokea timu ya Polisi FC ya nchini Rwanda pia.

Sanga alisema, wachezaji hao wanaondoka leo kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya kuungana na timu ya Singida United ambayo ipo kambini kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.
Singida United yasajili nyota wawili toka Rwanda Singida United yasajili nyota wawili toka Rwanda Reviewed by Zero Degree on 7/12/2017 08:28:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.