Loading...

Spika wa Bunge ametoa onyo kwa wanaoliita Bunge kuwa ni dhaifu.

Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai ametoa onyo kwa baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wakitumia lugha zisizofaa bungeni na kuliita bunge kuwa ni dhaifu.

Spika wa Bunge Mh Job Ndugai amesisitiza kuwachukulia hatua wabunge watakaokwenda kinyume na kanuni na taratibu za Bunge na kiti cha Spika likiwemo la kutumia lugha zisizo na staha katika Bunge.

Kamati ya pamoja ya Bunge inayojumuisha kamati za bunge nne yaani Kamati ya Madini,Kamati ya Katiba na sheria,Kamati ya sheria ndogo na kamati ya ardhi maliasili na mazingira imepokea taarifa ya miswada ya sheria mitatu ya mikataba ya rasilimali za nchi kutoka serikalini kupitia Waziri wa Katiba na sheria Prof Palamagamba Kabudi watakayoijadili na kuwasilisha bungeni baadae.

Miongoni mwa yatakayokuwamo katika miswada hiyo ni pamoja na kuboresha ushiriki na umiliki wa wananchi katika rasilimali za nchi lakini pia bunge kupewa nguvu ya kupitia mikataba ya madini kabla ya kusainiwa.
Spika wa Bunge ametoa onyo kwa wanaoliita Bunge kuwa ni dhaifu. Spika wa Bunge ametoa onyo kwa wanaoliita Bunge kuwa ni dhaifu. Reviewed by Zero Degree on 7/01/2017 09:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.