ACT - Wazalendo kuibwaga serikali mahakamani
Akizungumza kwenye mkutano na wananchi Mkoani Mwanza alipokuwa akifanya uzinduzi wa matawi tisa ya chama hicho, Zitto amesema wameamua kufanya hivyo kwa kuwa sheria ya vyama vya siasa haimtaji Rais mahali popote.
“Leo hii vyama tunahangaika hatupewi uhuru wa kufanya mikutano jana tumekubaliana tufungue kesi, tufungue kesi dhidi ya serikali ili mahakama itoe amri kuhusiana na nani mwenye haki kuzuia mikutano kwasababu sheria ya vyama vya siasa haimtaji Rais popote kwahiyo Rais hana mamlaka ya kutoruhusu mikutano isifanyike kwahiyo tumeamua kwenda mahakamani lakini haya mambo yalikuwa tangu mwaka 92 na waasisi wa mageuzi wa nchi hii leo miaka 20 baadae tunarudi nyuma eti vyama haviruhusiwi kufanya mikutano ili halikubaliki, halikubaliki, halikubaliki,” Alisema Zitto.
“Tunaomba wananchi mtupe ushirikiano bila vyama kufanya mikutano hamuwezi kujua nchi yenu inaendaje mambo ambayo Magufuli amesema mambo ya mikataba ya madini nyinyi mliyajua kwasababu sisi tuliyaibua ndani ya bunge leo Rais Magufuli anazungumzia masuala ya madini kwasababu sisi tuliyashughulikia miaka 10 iliyopita mambo ya Escrow si tulikuja kwenye mikutano kuwafafanulia? si mlifuatilia kwenye bunge ikiwa live, leo mnaona bunge likiwa live tusikubali kurudi nyuma juhudi za kuleta demokrasia kwenye nchi hii kwahiyo naomba muendelee kutuunga mkono na sisi tutapaza sauti hakuna mwanasiasa yoyote anaemkwamisha kiongozi yoyote katika kuleta maendeleo ya nchi, mendeleo ni ya wote.”
ACT - Wazalendo kuibwaga serikali mahakamani
Reviewed by Zero Degree
on
8/29/2017 12:47:00 AM
Rating: