Loading...

Hizi ndizo mechi watakazokosa Gary Cahill na Cesc Fabregas


Gary Cahill na Cesc Fabregas watakosa michezo kadhaa kufuatia kuonyeshwa kadi nyekundu wakati Chelsea ilipocheza dhidi ya Burnley.

Shirikisho la soka la Uingereza (FA) tayari imekwisha waadhibu rasmi wachezaji hao kwa mujibu wa kanuni na taratibu zao.

Nahodha huyo wa Chelsea pamoja na mwenzake wanatarajiwa kukosa moja ya michezo muhimu kwa klabu yao.


Cahill mwenye umri wa miaka 31 alipewa kadi nyekundu moja kwa moja kufuatia kumkabili vibaya Matt Lowton katika dakika ya 14 ya mchezo, sasa anatarajiwa kukosa mechi tatu.

Adhabu hiyo itamfanya Cahill kukosa katika mechi ya Chelsea dhidi ya Tottenham wikendi ijayo, pia ataikosa mechi ya Everton itakaoyochezwa Stamford Bridge wiki 
ijayo na ile ya Leicester City baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.


Fabregas yeye alipata kadi za njano mbili, moja ilikuwa baada ya madhambi aliyomfanyia Craig Pawson, na ya pili ilikuwa baada ya kufanya madhambi mengine. Cesc ataikosa mechi ya Chelsea dhidi ya Tottenham itayochezwa Jumapili ijayo kwenye uwanja wa Wembley, ambao utamuacha Conte katika wakati mgumu wa kufanya uchaguzi wa mtu atayecheza katikati siku hiyo.
Hizi ndizo mechi watakazokosa Gary Cahill na Cesc Fabregas Hizi ndizo mechi watakazokosa Gary Cahill na Cesc Fabregas Reviewed by Zero Degree on 8/15/2017 02:06:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.