Loading...

Makelele aibuka na ushauri huu kwa N'golo Kante


Makelele anadai, Kante anatakiwa kupunguza kasi kama anataka kuhimili katika ligi zote mbile, yaani Ligi Kuu ya Uingereza na katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Claude Makelele anafikiri kwamba, mshindi huyo wa tuzo ya mwaka iliyotolewa na PFA anaweza kujikuta anauchosha mwili wake na kushindwa kuhimili ligi zote ipasavyo endapo ataendelea kucheza katika kasi aliyonayo sasa.

Kante alijinyakulia tuzo kadhaa msimu uliopita na kuisaidia Chelsea kutwaa yyaji la Ligi Kuu ya Uingereza kwa mara ya tano katika historia ya klabu. Kiwango chake cha juu kilimfanya afananishwe na Makelele, lakini nyota huyo wa zamani wa 'The Blues' anasema kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 26 anaweza kwenda mbele zaidi na kupita kiwango hicho.


“Ni mchezaji mzuri. Ni vigumu kumpata mtu anayependa kukimbia ndani ya dimba kama yeye,” Makelele alisema. “Anacheza kwa ajili ya wenzake. Ana uwezo wa ajabu. Pia ni mwenye maarifa ya soka na huwa hana mzaha awapo uwanjani. Ukitazama wanaomzunguka nao wako vizuri, hivyo ana nafasi kubwa ya kuwa mchezaji bora zaidi."

“Inawezakuwa ngumu kwake baadae atakapo kuwa na umri mkubwa. Hatoweza kukimbia namna ile kwa muda wa dakika 90. Nafikiri siku moja itambidi abadilishe mfumo wake wa kucheza. Anaweza akatumia maarifa yake zaidi, na kuachana na kutumia kasi kubwa.

“Kama atataka kucheza vema kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, FA na Klabu Bingwa, anaweza akahitajika kufanya marekebisho kidogo kwenye kasi yake awapo uwanjani. Hata hivyo, Chelsea walimsajili aje kucheza kama ambavyo anacheza sasa kwa kasi kubwa. Hivyo hilo nalo ni tatizo.

“Ni muhimu kwa yeye kuelewa jinsi ya kuilinda nguvu yake. Bado ni mdogo kiumri, wakati atakapokuwa na umri mkubwa zaidiatakuja kuelewa namna ya kubadilisha aina yake ya mchezo.”
Makelele aibuka na ushauri huu kwa N'golo Kante Makelele aibuka na ushauri huu kwa N'golo Kante Reviewed by Zero Degree on 8/24/2017 02:10:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.