Loading...

Wafungwa wenye ujuzi na waliojirekebisha kitabia kuwezeshwa


Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Mwigulu Nchemba amesema serikali inaandaa utaratibu wa kuwawezesha wafungwa wenye ujuzi na walijirekebisha kitabia kuweza kujiajiri na hata kuajiriwa hatua itakayosaidia kuepuka kurudia makosa na pia kuongeza uzalishaji.

Waziri Mwigulu ameyasema hayo wakati wa anazindua Nyumba nne za Askari Magereza katika gereza la Kisongo liliyoko Jijini Arusha.

wakizungumza baada ya uzinduzi wa nyumba hizo zilizogharimu Milioni 260 viongozi na watendaji akiwemo Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Dr. Juma Malema na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha Hamis Nkubasi wamesema kukamilika kwa nyumba hizo ni sehemu ya mkakati wa Jeshi hilo wa kukabiliana na changamoto zilizopo na kuboresha huduma.

Mbunge wa Arusha Mh Godbless Lema amesema serikali ikiwatumia vizuri Wafungwa walioko ndani ya magereza unaweza kufanikisha mambo mengi yakiwemo kupata taarifa za mitandao ya uhalifu.
Wafungwa wenye ujuzi na waliojirekebisha kitabia kuwezeshwa Wafungwa wenye ujuzi na waliojirekebisha kitabia kuwezeshwa Reviewed by Zero Degree on 8/29/2017 08:09:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.