Loading...

Waziri Mkuu wa Algeria atumbuliwa


Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika amemtimua kazi Waziri Mkuu wake Abdelmadjid Tebboune (71), ambaye aliteuliwa katika nafasi hiyo miezi mitatu iliyopita.

Baada ya kutimuliwa kazi Waziri huyo tayari jina la Waziri mpya limetajwa la Ahmed Ouyahia kumrithi ambaye alikuwa mnadhimu mkuu wa Rais. Hakuna sababu zilizotajwa za kufukuzwa kazi Tebboune.

Siku kadhaa Rais Bouteflika alimtumia barua kali Tebboune kutaka kufanyika mabadiliko ya sera.
Waziri Mkuu wa Algeria atumbuliwa Waziri Mkuu wa Algeria atumbuliwa Reviewed by Zero Degree on 8/16/2017 06:24:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.