Loading...

FIFA yaizuia Leicester kumsajili mchezaji baada ya kuchelewa sekunde 14


Fifa wamelikataa ombi la Leicester City la kutaka kumsajili kiungo wa kati, Adrien Silva baada ya klabu hiyo kuchelewa kwa sekunde 14 kumaliza usajili wake kabla ya muda wa mwisho kufika.

Leicester walimnunua mchezaji huyo kutoka Sporting Lisbon kwa £22m lakini walikamilisha mkataba huo karibu sana na wakati wa kufungwa kwa dirisha la kuhama wachezaji tarehe 31 Agosti.

Usajili wa Silva kama mchezaji wa klabu hiyo katika shirikisho hilo linalosimamia soka duniani haukukamilishwa kwa wakati.

Hii ina maana kwamba mchezaji huyo ni wao lakini hawezi kuwachezea hadi dirisha lifunguliwe tena Januari.

Leicester wameanza mchakato wa kukata rufaa kufuatia uamuzi huo wa Fifa.

Msemaji wao amesema: "Tunafanya juhudi za Adrien na Sporting Clube de Portugal kutatua matatizo kuhusu usajili wa mchezaji huyo na tunajaribu kutafuta suluhu."

Klabu hiyo inammiliki Silva lakini kuna baadhi ya sehemu za mkataba ambazo hazikuwa zimekamailishwa kikamilifu.

Hii ina maana kwamba watahitajika kulipa ujira wake hadi wajaribu kukamilisha usajili wake kikamilifu Januari.

Silva, 28, ni mzaliwa wa Ufaransa na alikuwa kwenye akademi ya klabu ya Sporting.

Alicheza kwa mkopo Maccabi Haifa na Academica.

Amechezea Ureno mechi 20 za kimataifa na kuwafungia bao moja na aliwachezea waliposhinda Euro 2016.

Leicester pia walimuuza kiungo wa kati Danny Drinkwater kwa Chelsea kwa £35m dakika za mwisho kabla ya kufungwa kwa soko Alhamisi wiki iliyopita.
FIFA yaizuia Leicester kumsajili mchezaji baada ya kuchelewa sekunde 14 FIFA yaizuia Leicester kumsajili mchezaji baada ya kuchelewa sekunde 14 Reviewed by Zero Degree on 9/06/2017 01:39:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.