Hatimaye Chelsea wamefikia makubaliano na Atletico Madrid
Kwa mujibu wa taarifa ya SkySports, inaonesha Atletico watatakiwa kulipa zaidi ya paundi milioni 50 kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Spain, ambaye anatarjiwa kufanya vipimo vya afya Madrid.
Chelsea hawatahusika na swala la malipo ya Costa baada ya kuwa amesaini mkataba na Atletico.
Chelsea hawatahusika na swala la malipo ya Costa baada ya kuwa amesaini mkataba na Atletico.
Taarifa iliyotolewa na Klabu ya Chelsea inasema: "Klabu ya Chelsea leo imefikia makubaliano na Atletico Madrid kwa ajili ya uhamisho wa Diego Costa.
"Uhamisho utategemea vipimo vya afya na makubaliano binafsi baina ya mchezaji na timu."
Atletico walishindwa kulikazia mkazo suala la usajili wake kabla dirisha la usajili halijafungwa, ikiwa pia ni hofu kumshuhudia Costa akiwa benchi bila kuichezea timu hadi adhabu yao itakapokuwa imeisha mwezi Januari.
Costa hajacheza kwa muda wa siku 98 tangu aonekane kwa mara mwisho kwenye mechi ya Spain na Macedonia kwenye michuano ya kufuzu kushiriki kombe la dunia 2018.
Costa aliitumikia Atletico kwa miaka minne kabla hajajiunga na Chelsea mwezi Julai mwaka 2014 kwa paundi milioni 32.
Alifanikiwa kufunga magoli 59 ndani ya michezo 120 akiwa na Chelsea, ambapo katika kipindi hicho Chelsea imefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu mara mbili.
Hatimaye Chelsea wamefikia makubaliano na Atletico Madrid
Reviewed by Zero Degree
on
9/21/2017 05:56:00 PM
Rating: