Loading...

Mbunge CUF alivyowaponza madiwani wake


MADIWANI wanne wa Chama cha Wananchi (CUF) katika halmashauri ya Jiji la Tanga, wamesimamishwa kuhudhuria vikao vinne mfululizo na kukatwa posho zao za vikao baada ya kumsusia Mbunge wa chama hicho, Mussa Mbaruk na kutoka nje alipopewa nafasi ya kuzungumza.

Madiwani waliyosimamishwa na kata zao kwenye mabano ni Rashid Jumbe (Mwanzange), Khalid Hamza (Duga), Seleman Mbaruk ( Majengo), Mwasabu Ngale (Mabawa) na Abdrahaman Hassan (Msambweni).

Madiwani hao wamesimamishwa kuhudhuria vikao hivyo kutokana na kitendo chao cha kutoka nje ya ukumbi kususia hotuba ya mbunge huyo aliyepewa nafasi ya kutoa neno la shukrani kabla ya mstahiki meya kufunga kikao hicho

Kitendo cha madiwani hao kutoka nje ya ukumbi kwa lengo la kumsusia mbunge huyo kilisababisha Meya kuchukua hatua hizo kwa kilekilichoelezwa ni utovu wa nidhamu kwa kiongozi huyo.

Mbunge huyo aliwasha moto kwa kumtaka meya kuchukua hatua kali kwa madiwani hao na kueleza kuwa utovu huo wa nidhamu kwa viongozi hao ni kawaida yao hata kwenye vikao vya chama.

Hata hivyo, madiwani hao walirejea tena ukumbini baada ya mbunge huyo kumaliza kuzungumza na kuketi kwenye viti vyao jambo lililodhihirisha kutoka kwao nje ni kumsusia mbunge huyo.

Tukio hilo linajionyesha mgogoro unaofukuta ndani ya chama hicho taifa kati ya mwenyekiti anaetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim na Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharrif Hamad, umeanza kuleta athari kwa viongozi ngazi za chini kila upande kuushutumu mwingine kuwa ni kundi la wasaliti.

Katika kikao cha baraza hilo ambacho kilihudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tanga, Kassim Mbughuni, kilijadili masuala ya maendeleo pamoja na kuwasilishwa taarifa za kamati.

Baada ya wajumbe kuchangia hoja kwenye kamati hizo, Mbunge huyo alipewa nafasi ya kuzungumza kama mjumbe na wakati aliposimama madiwani hao walinyanyuka na kutoka nje licha ya kitendo hicho kukemewa na meya wa Jiji hilo, Mhina Mustaph.

Mwilapwa alisisitiza mshikamano na kuheshimiana viongozi na kuwakumbusha wajumbe wa baraza hilo kuwa migogoro kama hiyo ingesababisha kuvunjwa kwa baraza hilo, jambo ambalo lingerudisha nyuma harakati na mipango ya serikali ya kuleta maendeleo kwa wananchi.

Akitoa maamuzi kwa niaba ya wajumbe wa baraza hilo, Mustaph alitangaza kuwasimamisha vikao vitatu na kuwakata posho za vikao vinne.

Kwa upande wao madiwani hao walipinga adhabu hiyo wakidai hakuna kanuni yoyote inayompa mamlaka meya kumsimamisha mjumbe kwa kosa la kutoka nje kwa ajili ya kutomsikiliza mbunge au mjumbe wa kikao hicho.

Akizungumza kwa niaba ya wenazake, Jumbe ambaye ni mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Tanga, alisema kwa mujibu wa kanuni za mabaraza ya madiwani hakuna sehemu inayoagiza kusimamishwa kwa diwani kwa kutoka nje wakati mjumbe akiozungumza na kudai kuwa adhabu hiyo ni uhuni.

Alieleza wanaipinga adhabu na maamuzi yaliyotolewa na meya kwa kuwa hayana mantiki na wataendelea kuhudhuriavikao vijavyo kama wajumbe na hawakubaliani na adhabu hiyo aliyoiita ya kibabe na uhuni.
Mbunge CUF alivyowaponza madiwani wake Mbunge CUF alivyowaponza madiwani wake Reviewed by Zero Degree on 9/05/2017 06:40:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.