Loading...

Ripoti ya Makinikia kutua bungeni


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kesho anatarajiwa kukabidhiwa taarifa na Spika Job Ndugai za kamati mbili zilizoundwa na Bunge katika Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 kuhusu na makinikia ya almasi na biashara ya madini ya Tanzanite.

Kwa mujibu wa taarifa za bunge hafla fupi ya makabidhiano hayo itafanyika katika viwanja vya bunge na viongozi wa kitaifa watakuwepo. Kabla ya Waziri Mkuu kukabidhiwa taarifa hizo, kamati hizo mbili zitakabidhi taarifa zake kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye naye atakabidhi kwa Waziri Mkuu.

Kamati hizo zilizopewa siku 30 zimekamilisha kazi hiyo na zitawasilisha taarifa zao kesho,Septemba 6 mwaka huu. Katika tukio hilo, Mhe. Spika atapokea taarifa hizo na kuzikabidhi kwa Waziri Mkuu.

Katika Mkutano wa Saba wa Bunge la Kumi na Moja Mheshimiwa Spika aliunda Kamati Maalum mbili (2) kwa ajili ya kuchunguza biashara ya Madini aina ya Tanzanite na Almasi.
Ripoti ya Makinikia kutua bungeni Ripoti ya Makinikia kutua bungeni Reviewed by Zero Degree on 9/05/2017 11:22:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.