Loading...

'Serikali ipo tayari kugharamia matibabu ya Tundu Lissu' - Waziri Ummy


Serikali imesema ipo tayari kugharamia matibabu ya Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu ambaye kwa sasa hivi yupo Jijini Nairobi kwa matibabu kufuatiwa shambulio alilolipata Septemba 7, mwaka huu Mkoani Dodoma.

Hayo yamesemwa Jijini Tanga na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

Waziri Ummy Mwalimu alisisitiza Serikali inasubiri kupata maombi kutoka kwa familia ya mgonjwa ikiambatana na taarifa rasmi kutoka kwa madaktari kuhusu mahitaji ya matibabu zaidi ya mgonjwa ”Serikali ipo tayari kugharamia matibabu zaidi ya Mhe.Lissu popote Duniani”.

Akiwa kama Mtanzania na Mbunge,Serikali inayo wajibu wa kugharamia matibabu yake hadi apone ili aweze kuendelea na kazi ya kuwahudumia Watanzania na wana Singida Mashariki.

Serikali inapenda kusisitiza kwamba iko tayari kuendelea kushughulikia matibabu endapo maombi ya kufanya hivyo yatawasilishwa rasmi Serikalini,ikiwemo kupata taarifa ya maendeleo ya afya yake kutoka kwa Madaktari wanaomhudumia hapo Nairobi ambayo itatakiwa kupatikana
kupitia ridhaa itakayotolewa na Mhe. Lissu au Mwanafamilia wa karibu kama taratibu za Kidaktari zinavyoelekeza.


Aidha, Serikali imeshangazwa na dhana ya kuchangishana kwa ajili ya matibabu ya Mhe. Lissu, kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kutokea matapeli watakaochangisha Watanzania fedha kwa madai kwamba Mbunge huyo amekosa hela za matibabu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anawashukuru Madaktari na watoa huduma wote wa Hospitali ya Rufaa Dodoma kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya katika kuokoa maisha ya Mhe.Lissu na kumtakia apate nafuu haraka
'Serikali ipo tayari kugharamia matibabu ya Tundu Lissu' - Waziri Ummy 'Serikali ipo tayari kugharamia matibabu ya Tundu Lissu' - Waziri Ummy Reviewed by Zero Degree on 9/21/2017 07:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.