Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Tarehe 22 Septemba, 2017


Manchester City wahofia kushindwa kumnasa Alexis Sanchez baada ya PSG kuonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo.

Klabu za Chelsea and Manchester United zina nafasi ndogo sana ya kuweza kumnasa nyota wa Bayern Munich, Rafinha wakati akiendelea kuonekana bora zaidi akiwa na klabu yake hiyo ya Ujerumani. (Chanzo: The Sun)

Arsene Wenger ameweka wazi kwamba alikuwa na nia ya kumsajili Gareth Barry mwaka 2009 wakati mchezaji huyo alipokuwa anaichezea klabu ya Aston Villa ya Uingereza. (Chanzo: Daily Telegraph)

Diego Costa anaweza kutangazwa rasmi kama mchezaji wa Atletico Madrid kabla Chelsea hawajasafiri kwenda Spain kukipiga na Klabu hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa baada ya Chelsea kukubali kumuuza kwa paundi milioni 60.

Star wa Timu ya wanawake ya Uingereza, Jodie Taylor anatarajiwa kuondoka Arsenal mwishoni mwa mwaka. (Chanzo: Daily Mail)
Pierre-Emerick Aubameyang asisitiza kwamba ndoto zake za kuhamia Real Madrid zimeshakufa. (Chanzo: The Star)

Arsene Wenger ameeleza kwamba hana mpango tena wa kumsajili beki wa West Brom, Jonny Evans. (Chanzo: Dily Express)

Harakati za Manchester United kumsajili Antoine Griezmann zimeingia doa, kwa Atletico kuonyesha nia ya kumbakiza ili ashirikiane na Diego Costa.

Arsenal wameingilia vita ya Liverpool na Manchester City kuwania saini ya kiungo wa Schalke, Leon Goretzka.

Liverpool wanamfuatilia beki wa RB Leipzig, Dayot Upamecano lakini inaonekana kwamba bei yake iko juu zaidi. (Chanzo: Daily Mirror)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Tarehe 22 Septemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Tarehe 22 Septemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 9/22/2017 10:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.