Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Tarehe 25 Septemba, 2017


Manchester United wanatarajia kuanza mazungumzo na David De Gea juu ya mkataba mpya na wanamatumaini makubwa kwamba atakubali kubakia klabuni licha ya kwamba Real Madrid imekuwa ikionesha nia ya kumsajili kwa muda mrefu. (Chanzo: The Independent)

Everton walikuwa tayari kulipa paundi milioni 70 kumnasa Diego Costa kabla ya nyota huyo kuelekea Atletico Madrid.

Arsene Wenger amewaonya makocha wenzake, Jose Mourinho na Pep Guardiola kwamba hakuna meneja mwenye uwezo wa kufuta michuano ya vikombe.

Jurgen Klopp anasisitiza kwamba mashabiki wa Liverpool tayari wamemsamehe Coutinho kwa kuomba kuondoka klabuni. (Chanzo: Daily Mirror)

Arsene Wenger amesema kwamba kurejea kwa Kieran Gibbs Arsenal itakuwa kama muunganiko wa wanafamili waliopoteana.

Slaven Bilic yuko hatarini kutimuliwa kwenye kibarua West Ham baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Spurs wikendi iliyopita.

Pep Guardiola amepoteza matumaini ya kikosi chake kunyakua ubingwa na kukiri kwamba Ligi Kuu ya Uingereza ni ngumu zaidi kuliko mategemeo yake.

Kevin De Bruyne ameonyesha nia ya kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Manchester City kufuatia kupewa nafasi ya kuwaminika na kocha wake, Pep Guardiola kwenye kikosi cha kwanza. (Chanzo: Telegreph)

Manchester City wako tayari kuonyesha imani yao kwa nyota wao, Raheem Sterling kwa kumuongeza mkataba. 
(Chanzo: Daily Star)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Tarehe 25 Septemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Tarehe 25 Septemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 9/25/2017 09:29:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.