Loading...

Courtois amtetea Antonio Conte


Mlinda mlango wa klabu ya Chelsea, Thibaut Courtois anasema meneja wao, Antonio Conte hana tatizo lolote na wachezaji kama inavyodhaniwa.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza walifanikiwa kupata ushindi wao wa kwanza wa goli 4-2 dhidi ya Watford wikendi iliyopita baada ya kushindwa kupata matokeo mazuri katika michezo mitatu mfululizo iliyotangulia kabla, lakini kibarua cha Conte kilioneka kuwa mashakani kabla ya mchezo huo uliochezwa Jumamosi.


Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo, Courtois alisema: "Wakati wowote timu kubwa inapokuwa na matokeo mabaya, jambo la kwanza ambalo watu husema ni kwamba, wachezaji hawamtaki kocha na hawafuati maelekezo yake."

"Lakini tulipocheza dhidi ya Watford, uliona jinsi tulivyojituma kwa nguvu zetu zote muda wote na tulipigania kubadilisha matokeo tukitokea nyuma, hivyo kila mtu anaweza kuona kwamba tuko pamoja na kocha wetu.

"Uvumi kama huo ni rahisi sana kusambaa kila kona lakini sidhani kama kuna ukweli wowote. Kama mtu anakuwa hana furaha, nafikiri ataweka wazi badala ya kwenda kusema kwa vyombo vya habari, hivyo sio kweli.

"Kwanza kabisa, ni kazi ya wachezaji kuipigania timu ipate matokeo mazuri uwanjani. Kwa sasa ni suala la kukimbizana, kupambana na kupigania mpira zaidi ya kuonyesha manjonjo."

Chelsea wataikaribisha Everton Stamford Bridge kwenye michuano ya Carabao ikiwa ni siku moja imepita tangu meneja wa klabu ya Everton, Ronald Koeman afukuzwe kazi, lakini Courtois anatambua kwamba timu hiyo sio ya kubeza.

"Ni michuano ya kuwania kikombe na kwa hali hiyo, kila mtua atajaribu kushinda ili asonge mbele zaidi," aliongeza Courtois.

"Unajikuta unataka kwenda mbele zaidi. Na majeruhi tulionao, labda hatuna nafasi ya kujipanga sawa sawa tusubiri tuone kocha atapanga kikosi gani, lakini sidhani kama ni mchezo wa kubeza.

"Kwenye Ligi Kuu tuanatakiwa kupigana ili tuendelee kupata matokeo mazuri kwa kushinda mechi nyingi zaidi na Michuano ya Carabao ni kitu kingine, hivyo tunapaswaa kujaribu kufanya lile linawezaekana na kusonga mbele zaidi.

"Everton wamekua na wakati mgumu kwa sasa. Sidhani kwamba wanacheza vibaya ingawa wamefungwa magoli ya ovyo, na tunaweza kusema labda klabu nyingine zimekua na bahati tu, lakini kiufupi Ligi Kuu ni ngumu.

"Hata hivyo, hii ni michuano mingine na watakuwa tayari kushinda."
Courtois amtetea Antonio Conte Courtois amtetea Antonio Conte Reviewed by Zero Degree on 10/24/2017 11:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.