Loading...

Injini ya ndege ya abiria ya Air France yaharibika ikiwa angani


Ndege moja kubwa ya abiria ya AirFrance, muundo wa Airbus 380, imelazimika kutua kwa dharura baada ya injini yake moja kuharibika vibaya, ndege hiyo ikiwa angani.


Ndege hiyo superjumbo ilikuwa njiani kuelekea Los Angeles- Marekani kutoka mji mkuu wa Ufaransa- Paris, ikiwa na zaidi ya abiria 500.

Iliamua kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Goose Bay, mashariki mwa Canada.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika kisa hicho, lakini abiria walisalia ndegeni kwa saa kadhaa, baada ya ndege hiyo ya abiria kutua.

Wakati wa kisa hicho, ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 496 na wafanyikazi 24. Hayo ni kwa mjibu wa msemaji wa Air France spokesperson, aliyezungumza na shirika la habari la AFP.
Injini ya ndege ya abiria ya Air France yaharibika ikiwa angani Injini ya ndege ya abiria ya Air France yaharibika ikiwa angani Reviewed by Zero Degree on 10/01/2017 09:19:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.