Loading...

Mechi atakazozikosa N'Golo Kante wakati anaendelea kujiuguza


N'Golo Kante anatarajiwa kuonekana uwanjani baada ya wiki sita kufuatia majeraha aliyopata kwenye michuano ya kufuzu Kombe la Dunia.

Chelsea walipata pigo jingine wakati wa michuano ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 kufuatia kuumia kwa kiungo wao tegemezi, Kante anayehofiwa kukaa benchi kwa muda wa wiki sita kwa sababu ya majeraha aliyopata wakati anaitumikia timu yake ya Taifa ya Ufaransa.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, ni mojawapo ya wachezaji wa muhimu katika kikosi cha Conte, na kuna uwezekano akakosa michezo miwili ya Ligi ya Mabingwa pamoja na mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Manchester United tarehe 5 Novemba.


Antonio Conte tayari anaye Morata kwenye benchi akiwa na tatizo kama hilo la Kante na sasa ana wakati mgumu kupambana na hali ya kikosi chake kufuta pengo la kiungo huyo.
Mechi atakazozikosa N'Golo Kante wakati anaendelea kujiuguza Mechi atakazozikosa N'Golo Kante wakati anaendelea kujiuguza Reviewed by Zero Degree on 10/13/2017 02:28:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.