Miss Tanzania 2017 anusurika
Kwa mujibu wa taarifa ya Gazeti la Ijumaa, Diana ambaye kiasili ni Mmasai alisema kuwa, tukio hilo hatalisahau kwa kuwa alifanikiwa kuchoropoka mikononi mwa ndugu zake hao waliotaka kuhakikisha anafanyiwa tohara hiyo kama wenzake. “Kwa mila za kwetu mwanamke ukifikia umri fulani ni lazima afanyiwe ukeketaji.”
Kwangu mimi sikutaka kabisa kitu kama hicho kinitokee lakini kitendo cha kutia mguu nyumbani kwetu hivi karibuni huko Sakina, ndugu pamoja na watu wengine walinifuata na kunitaka nikeketwe, kisa kutimiza mila.
“Hata hivyo, nilifanikiwa kutoka mikononi mwao japokuwa hadi sasa hivi bado kuna ndugu wanaendelea kushikilia msimamo wa mimi kufanyiwa hivyo, lakini mwisho wa yote sikukubali kufanyiwa mambo yaliyopitwa na wakati,” alisema Diana huku akilengwa na machozi.
Diana alikuwa Miss Tanzania mwaka jana katika kinyang’anyiro kilichofanyika jijini Mwanza akiiwakilisha Wilaya ya Kinondoni.
Miss Tanzania 2017 anusurika
Reviewed by Zero Degree
on
10/13/2017 02:33:00 PM
Rating: