Loading...

Morata ataja sababu tatu za kuichagua Chelsea na si Manchester United


Alvaro Morata ametaja sababu tatu zilizompelekea aichague Chelsea dhidi ya Manchester United.

Kufuatia kurejea Real Madrid akitokea Juventus, Mhispania huyo alishindwa kutulia Bernabeu na mwisho wa siku akasajiliwa na Chelsea kwa kiasi cha paundi milioni 60.

Kipindi chote cha majira ya joto kilichopita, nyota huyo mwenye umri wa miaka 25, alikuwa anahusishwa na kujiunga na Manchester United na hata kufikia hatua ya kupaka rangi nyekundu kwenye nywele zake.

Lakini, akizungumza kabla ya mchezo wa Chelsea wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Roma, Morata alifichua siri kwa kusema kwamba, suala la kuhamia Chelsea lilikuwa limeshapangiliwa tangu mwanzo.


Kwa mujibu wa taarifa ya 'Gazetta dello Sport', Morata alisema: "Nilikuja kwa sababu kulikuwa na kocha kama Antonio Conte,"

 “Tulianza kuzungumzia kuhusu suala la uhamisho masika iliyopita na mwisho wa siku nikatua ndani ya mji wa London.

"Ninadaiwa na Antonio Conte. Yeye alinichukua kutoka Real kenda Juve kisha akawa ameenda kuinoa timu ya Taifa ya Italia. Nilipofahamu kwamba ananihitaji tu, sikufukilia mara mbili"

"Kulikuwa na sababu kadhaa zililozonivuta Chelsea," aliongeza. "Kwanza ilikuwa ni Kocha: Nilijua kabisa kwamba ninauweza mfumo wa Antonio Conte.

"Pili, ni mazingira: Nilipokelewa vizuri na jamaa zangu. Uwepo wa Wahispania wenzangu, na pia watu kama Azplicueta, Alonso, Fabregas na Pedro, ulinirahisihia maamuzi.

"Tatu, ni mke wangu, Alice Campello: Alikuwa tayari kunifuata London."
Morata ataja sababu tatu za kuichagua Chelsea na si Manchester United Morata ataja sababu tatu za kuichagua Chelsea na si Manchester United Reviewed by Zero Degree on 10/31/2017 03:22:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.