Loading...

Orodha ya wanawake matajiri zaidi duniani mwaka 2017

Alice Walton
Mfaransa Liliane Bettencourt, 94, wa maduka ya bidhaa za urembo L'Oreal, alikuwa ndiye mwanamke tajiri zaidi duniani akiwa na mali ya $39.5bn. Alirithi biashara hiyo.

Lakini alifariki dunia mwezi uliopita. Sasa ni nani mwanamke tajiri zaidi duniani?

Nafasi hiyo imechukuliwa na Alice Walton, ambaye ana mali ya jumla ya $33.8bn, $1.5bn juu ya mwaka jana. Kwa jumla, alishikilia nambari 17 katika orodha ya mabilionea wa Forbes waliotanagzwa mapema mwaka huu.

Watson ambaye ni binti pekee wa mwanzilishi wa maduka ya Wal-Mart Sam Walton, ndiye mwanamke tajiri zaidi Marekani.

Utajiri wake unatokana na hisa zake katika Wal-Mart pamoja na malipo ya mgawo wa faida.

Yeye ni miongoni mwa wanawake wanne wa familia ya Walton ambao wamo kwenye orodha ya wanawake matajiri zaidi duniani, kwa pamoja utajiri wao ukiwa jumla ya $49.5 bilioni. Wanne hao ni Christy Walton, mjane wa kakake John, na binamu zake Anne Walter Kroenke na Nancy Walton Laurie.

Jacqueline Mars, mwenye mali ya $27 bilioni na ambaye babu yake Frank Mars alianzisha kampuni ya pipi ya Mars Inc ndiye mwanamke wa tatu kwa utajiri duniani.

Maria Franca Fissolo anamfuata akiwa na mali ya $25.2 bilioni.

Mumewe marehemu Michele Ferrero alianzisha kampuni ya Ferrero Group. Kampuni ya Ferrero hutengeneza Ferrero Rocher, Kinder Chocolate na Tic Tacs. Kampuni hiyo pia ndiyo hutengeneza Nutella.


Isabel dos Santos kutoka Angola ndiye mwanamke tajiri zaidi Afrika
Isabel dos Santos kutoka Angola bado ndiye mwanamke tajiri zaidi Afrika, na utajiri wake unakadiriwa kuwa $3.1 bilioni.
Mjane wa Steve Jobs

Mjane wa Steve Jobs, Laurene Powell Jobs, ambaye ana utajiri wa $20 bilioni kutokana na hisa zake katika kampuni za Apple na Disney ni wa tano kwenye orodha hiyo ya wanawake matajiri.

Wengi wa wanawake matajiri duniani walirithi utajiri wao, kwa mujibu wa Forbes.

Lakini pia wapo wafanyabiashara 15 wa kike ambao hawakurithi mali, sana kutoka Asia.

Mmoja ni Nguyen Thi Phuong Thao kutoka Vietnam anayemiliki kampuni ya safari za ndege ya VietJet.

Marekani, ambayo ina mabilionea wengi wanawake duniani, ina wanawake 74 mabilionea.

Ujerumani na Uchina zinafuata zikiwa na mabilionea 28 na 23.


Wanawake matajiri zaidi duniani 2017

1. Alice Walton - $33.8bn


Utajiri: Wal-Mart

2. Jacqueline Mars - $27bn

Chanzo cha Utajiri: Pipi

3. Maria Franca Fissolo - $25.2bn

Chanzo cha Utajiri: Nutella, chokoleti

4. Susanne Klatten - $20.4bn

Chanzo cha Utajiri: BMW, dawa

5. Laurene Powell Jobs - $20bn

Chanzo cha Utajiri: Apple, Disney


6. Gina Ronehart - $15bn

Chanzo cha Utajiri: Uchimbaji madini

7. Abigail Johnson - $14.4bn

Chanzo cha Utajiri: Usimamizi wa fedha

8. Iris Fontbona - $13.7bn

Chanzo cha Utajiri: Uchimbaji madini

9. Beate Hesiter - $13.6bn

Chanzo cha Utajiri: Maduka ya jumla

10. Charlene de Carvalho-Heineken - $12.6bn

Chanzo cha Utajiri: Heineken

11. Blair Parry-Okeden - $12.2bn

Chanzo cha Utajiri: Vyumba vya habari

12. Massimiliana Landini Aleotti - $9.5bn

Chanzo cha Utajiri: Dawa

13. Yang Huiyan - $9bn

Chanzo cha Utajiri: Biashara ya nyumba na ardhi

14. Katharine Rayner - $8.1bn

Chanzo cha Utajiri: Vyumba vya habari

15. Margaretta Taylor- $8.1bn

Chanzo cha Utajiri: Vyumba vya habari

16. Zhou Qunfei: - $7.4bn

Chanzo cha Utajiri: Skrini za simu za kisasa

17. Pauline MacmMillan Keinath - $6.8bn

Chanzo cha Utajiri: Cargill

18. Sandra Ortega Mera - $6.7bn

Chanzo cha Utajiri: Zara

19. Carrie Perrodo - $6.3bn

Chanzo cha Utajiri: Mafuta
Orodha ya wanawake matajiri zaidi duniani mwaka 2017 Orodha ya wanawake matajiri zaidi duniani mwaka 2017 Reviewed by Zero Degree on 10/17/2017 08:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.