Loading...

Ronaldo hatarini kufungiwa kwa kitendo alichomfanyia kiungo wa Girona


Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane atalazimika kutafuta mbadala wa Cristiano Ronaldo kikosini kwa mara ya pili katika msimu huu.

Mchezaji bora wa FIFA, Cristiano Ronaldo alikosa michezo mitano ya Real Madrid baada ya kutolewa nje kwa kujiangusha na kisha kumsukuma mwamuzi wakati wa mchezo wao dhidi ya Barcelona.

Hadi hivi sasa, winga huyo wa klabu ya Real Madrid amefunga goli moja kwenye La Liga.

Real Madrid walianza msimu kwa kupata matokeo mabaya, hali ambayo imeendelea kuonekana hadi jana Jumapili, walipofungwa goli 2-1 na timu iliyopanda daraja msimu huu, Girona.

Lakini mambo yanakuwa mabaya kwa mshambuliaji wa Real Madrid raia wa Ureno, ambaye yuko hatarini kufungiwa michezo kadhaa baada ya kuonyesha kitendo cha utovu wa nidhamu.

Ronaldo alionekana akikabiliana na kiungo wa Girona, Pere Pons kwenye kona ya uwanja.


Wakati mpira ulipopigwa kuelekea alipokuwa na yeye kugundua kuwa hawezi tena kuucheza kwa kichwa chake aliachana na mpira kisha akamwangusha chini kiungo huyo kwa kumsuka kichwani, huku mpira ukichezwa na beki mwingine wa Girona.

Kwa hivi sasa, Real Madrid wako nyuma kwa pointi nane dhidi ya viongozi Ligi, FC Barcelona kwenye michuano ya La Liga na kuna uwezekano mkubwa wa kumkosa mshambuliaji wao Cristiano Ronaldo katika mechi kadhaa.
Ronaldo hatarini kufungiwa kwa kitendo alichomfanyia kiungo wa Girona Ronaldo hatarini kufungiwa kwa kitendo alichomfanyia kiungo wa Girona Reviewed by Zero Degree on 10/30/2017 12:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.