Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 20 Octoba, 2017
Wachezaji wa Chelsea wanadai mazoezi wanayopewa na kocha wao, Antonio Conte ni mazito na kudai kwamba yanachangia kwa kiasi kikubwa klabu kuandamwa na majeruhi pia itawawea vigumu kutetea ubingwa wao. (Chanzo: Times)
Umaro Embalo |
Manchester United walivutiwa na kiwango cha kinda wa Benifica, Umaro Embalo kwenye Ligi ya Mabingwa kati ya pande hizo mbili (Benifica Vs Man U) usiku wa juzi Jumatano na hivyo wanaweza kujaribu kumsajili kinda huyo pamoja na mwenzake Joao Felix.
Juan Mata, Ander Herrera, Marouane Fellaini na Phil Jones wanatarajiwa kusaini mikataba mipya na klabu ya Manchester United.
Klabu za Barcelona na Real Madrid kuingia vitani kusaka saini ya kinda mwenye umri wa miaka 16 kutoka Brazil, Lincoln, ambaye amekua gumzo kwenye michuano ya kombe la dunia chini ya miaka 17. (Chanzo: Sun)
Mesut Ozil ana uhakika wa kujiunga na klabu ya Manchester United ifikapo mwezi Januari na tayari ameshaanza kuwaeleza baadhi ya wachezaji wenzake juu ya mpango huo. (Chanzo: Daily Mirror)
Liverpool hawako tayari kupokea ofa yoyote kutoka klabu nyingine za Ligi Kuu ya Uingereza kwa ajili ya James Milner pamoja na kwamba nafasi ya kudumu kikosini imechukuliwa na Alberto Moreno. (Chanzo: Telegraph)
Barcelona walimwagiza mkurugenzi wao wa michezo, Robert Fernandez kwenda kuwachunguza Harry Kane na Christian Eriksen wakati wa mechi ya Tottenham ya Ligi ya Maingwa dhidi ya Real Madrid Jumanne.
Wachezaji wa Leicester hawajafurahia kufukuzwa kazi kwa kocha wao, Craig Shakespeare na kuomba maelezo zaidi kutoka kwa uongozi wa juu kabla ya jana Alhamis.
Arsenal na Chelsea wako katika mawindo ya saini ya winga wa klabu ya Brest ya Ufaransa, Lenny Pintor.
Aliyekuwa kiungo wa zamani wa Chelsea, Ramires atajiunga na Inter Milan kwa mkopo mwezi Januari akitokea Jiangsu Suning ya China. (Chanzo: Daily Mail)
Real Madrid wanajutia kutomuuza Bale wakati wa majira ya joto, kitu ambacho kinaaminika kingeweza kufanikisha usajili wa Kylian Mbappe. (Chanzo: Star)
Neymar aliwaambia wenzake kuhusu mpango wake wa kuhamia PSG wakati wa harusi ya Lionel Messi.
Divock Origi anadai kwamba hajawahi kuwasiliana na meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp tangu ajiunge na klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani kwa mkopo katika majira ya joto. (Chanzo: Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 20 Octoba, 2017
Reviewed by Zero Degree
on
10/20/2017 11:29:00 AM
Rating: