Loading...

Yusuf Manji aingia matatani tena


Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji ameendelea kuingia matatani baada ya Kampuni ya Udalali ya Yono kuzifunga ofisi zake zilizopo Barabara ya Pugu.

Yono wamezifunga ofisi na maghala ya Manji ambaye alikuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga akituhumiwa kudaiwa kodi ya zaidi ya Sh300 milioni na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kwa mujibu wa taarifa ya Gazeti la Mwananchi, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Yono, Scholastika Kevela alisema, ‘‘ni kweli tumezifunga ofisi za Manji zilizopo eneo la Pugu, anadaiwa fedha nyingi za kodi na TRA.” 

Alipoulizwa kipi kitafuata baada ya kuzifunga, Kevela alisema, ‘‘sisi utaratibu wetu ni kwamba tukizifunga huwa tunatoa siku 14 mhusika akalipe na baada ya hapo sasa tunasubiri maelekezo kutoka kwa TRA.”
Yusuf Manji aingia matatani tena Yusuf Manji aingia matatani tena Reviewed by Zero Degree on 10/28/2017 09:22:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.