Loading...

Kocha wa West Bromwich, Tony Pulis atimuliwa kazi

Pulis afukuzwa kazi West Brom
Utawala wa Tony Pulis katika klabu ya West Bromwich Albion umefika kikomo baada ya uongozi wa klabu hiyo kumfukuza kazi meneja huyo mwenye umri wa miaka 59 na nafasi yake inachukuliwa na msaidizi wake, Gary Megson kwa muda.

West brom hawajashinda mechi yoyote tangu mwezi Agosti na walikubali kichapo cha goli 4-0 kutoka kwa Chelsea katika uwanja wao wa nyumbani Jumamosi.

Tony Pulis
Pulis alifanikiwa kuipatia West brom
 ushindi wa mechi 36 kati ya 121 na kupoteza mechi 49, rekodi itakayochukuliwa kama mojawapo ya rekodi zake mbovu katika maisha yake ya umeneja. Ni timu tatu pekee za Ligi Kuu ya Uingereza zilizofunga magoli chini ya 9 kama West brom.

Hii hapa ni kauli iliyotolewa na klabu ya Westbrom:

“Uamuzi huu haujachukuliwa kirahisi kamwe lakini siku zote ni kwa maslahi ya klabu.

“Tunazungumzia matokeo na kwa kipindi cha msimu uliopita na huu tulionao sasa, kwetu umekuwa wa kukatisha tamaa sana.

“Tungependa kuweka rekodi ya kutambua mchango wa Tony na kazi ngumu aliyoifanya katika kipindi cha mpito kilichoambatana na maabadiliko ya umiliki wa klabu. Tunamtakia maisha mema katika siku zake zijazo.”

Hakika Pulis atarejea kibaruani mapema iwezekanavyo kwani hajawahi kukaa bila kazi kwa muda mrefu tangu mwaka 2002 na kabla ya hapo kulikuwepo na tetesi nyingi zilizodai meneja huyo anawindwa na vilabu kadhaa vya Ligi Kuu ya Uingereza.
Kocha wa West Bromwich, Tony Pulis atimuliwa kazi Kocha wa West Bromwich, Tony Pulis atimuliwa kazi Reviewed by Zero Degree on 11/20/2017 06:37:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.