Loading...

Majibu ya Eden Hazard alipoulizwa kama angependelea kuhamia Real Madrid

Eden Hazard adai ataondoka Chelsea atakapokuwa tayari
Hazard amesema yeye ni mshabiki wa klabu ya Real Madrid, lakini ataondoka Chelsea atakapokuwa tayari.

Mbelgiji huyo hakulazimisha kuondoka katika dirisha la usajili lililopita kama ambavyo vyombo vya habari vilidai na bado anasistiza kwamba anafurahia kuwa Stamford Bridge.

Hata hivyo, amesema hana mpango wa kukaa Chelsea kwa muda mrefu, akidai kwamba ataondoka pale atakapojisikia kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya kituo kimoja cha utangazaji nchini Ufaransa, Hazard alisema: “Siku zote najisikia vizuri nikiwa katika klabu hii.

“Bado nina miaka miwili katika mkataba wangu.

“Nitakapojisikia kuondoka, nitaondoka. Lakini, kwa sasa mimi ni wa Chelsea.

“Tunafahamu kuwa naipenda klabu ya Real Madrid, lakini niko Chelsea. Kila mwaka walisema nitaondoka lakini nilibakia katika klabu yangu.

“Nilipokuwa Lille, ilitangazwa ningehamia Paris lakini haikuwa hivyo. Watu walisema hivyo pia na hapa Chelsea, lakini bado nipo.”

Mkataba wa sasa wa Hazard unambakisha London hadi itakapofika mwezi Juni mwaka 2020 lakini alidai anaweza kushawishika kuhamia Real Madrid katika majira ya joto.

Eden Hazard
Alipoulizwa kama angependelea kuhamia Real Madrid, alijibu kwa ufupi: “Bila shaka, ni hayo tu.

“Kila mtu ana ndoto zake. Bila shaka, nitafikiria hivyo kama Madrid watatoa ofa.

“Matamanio yangu ni kushinda mataji ya kutosha na itakuwa vizuri zaidi kushinda Taji la Ligi ya Mabingwa.”
Majibu ya Eden Hazard alipoulizwa kama angependelea kuhamia Real Madrid Majibu ya Eden Hazard alipoulizwa kama angependelea kuhamia Real Madrid Reviewed by Zero Degree on 11/24/2017 06:36:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.