Loading...

Mshambuliaji wa Watford anayegombewa na Arsenal, Tottenham na Chelsea


Ripoti za hivi akribuni zinadai kwamba, Arsenal, Tottenham na sasa Chelsea zote zinatamani kupata saini ya mshambuliaji wa Watford, Richarlison.

Richarlison
Richarlison ana magoli manne katika mechi 11 za Ligi Kuu ya Uingereza na amekuwa kivutio cha wengi kwa uwezo aliouonyesha msimu huu.

Meneja wa Watford, Marco Silva haonyeshi kushangazwa kwa kitendo cha Mbrazil huyo kupendwa na klabu kubwa kama vile Chelsea na Tottenham.

Keulekea mechi ya Watford dhidi ya West Ham, Silva aliwaambia Waandishi wa Habari kwamba: “Sio jambo la kushangaza,” 

“Ameifanyia Timu yetu mambo ya ajabu na Ligi Kuu ya Uingereza kwa ujumla. Ni jambo la kawaida kila mtu kuanza kumzungumzia, jambo la muhimu ni kwamba anatakiwa kukuza kiwango chake.

“Ni mchezaji mwenye kiwango cha juu, hivyo ni kawaida kwa kila mtu kuanza kumzungumzia.

“Yuko tofauti na mchezaji wa kawaida wa Brazil; kwa mahitaji ya timu yetu, ni mchezaji mwenye ujuzi tunaouhitaji.

“Hapa tunazungumzia mchezaji mwenye kipaji kikubwa sana. Nina uhakika huko mbeleni atakuja kufikia mafanikio yote anayotaka.”
Mshambuliaji wa Watford anayegombewa na Arsenal, Tottenham na Chelsea Mshambuliaji wa Watford anayegombewa na Arsenal, Tottenham na Chelsea Reviewed by Zero Degree on 11/20/2017 12:01:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.